TECEC News and Events

Maji ya kunywa Darasa la Awali labadili maisha

Jina langu ni Neema, mimi ni mwanafunzi wa miaka 4 wa shule ya awali katika Shule ya Msingi ya Wita. Nataka kukueleza jinsi TECEC imebadilisha maisha yangu.

Kabla TECEC hawajaja, darasa letu la awali halikuwa na ndoo ya maji safi ya kunywa. Mara nyingi tulipaswa kuleta maji yetu kutoka nyumbani, jambo ambalo lilikuwa gumu kwa baadhi yetu, na mara nyingine maji ya kunywa hayapatikani nyumbani. Hii ilikuwa sio tu usumbufu bali pia hali isiyo ya usafi.

mambo yalibadilika na kuwa mazuri wakati TECEC ilipotupatia ndoo ya maji safi ya kunywa, ambayo walimu wetu hutuwekea maji ya kunywa muda wote tukiwa darasani. Inaweza kuonekana kama kitu kidogo, lakini kwetu sisi, imeleta mabadiliko makubwa.

Kwanza, kuwa na maji safi darasani kumeboresha afya yetu na ustawi kwa ujumla. Hatuwi tena na wasiwasi wa kuugua kutokana na kunywa maji machafu au kukauka kwa ajili ya kiu, Tunajisikia wachangamfu na nguvu, ambayo inatusaidia kusoma vizuri darasani na kushiriki kikamilifu katika shughuli mbalimbali.

Asante sana!

Neema
Made on
Tilda